Azam yakula bao la ugenini Ethiopia Kombe la Shirikisho Afrika

119

Azam FC leo Jumapili imepoteza mchezo wa awali wa Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufungwa mtanange dhidi ya Fasil Kenema kwa goli 1-0 mchezo uliopigwa Ababa Ethiopia.

Mchezo huu umechezwa uwanja wa Bahir, Dar, nchini Ethiopia na bao la ushindi lilipatikana kipindi cha kwanza dakika ya 45 +2 kupitia kwa Bezabeth Meleyo.

Licha ya nguvu za wachezaji wa Azam FC kupata bao la kusawazisha kipindi cha pili ziligonga mwamba huku wakishuhudia mpira ukigonga mwamba mara mbili, mpaka dakika tisini zinakamilika Azam walikuwa nyuma kwa goli moja kwa bila.

Mchezo wa marudio utachezwa kati ya Agosti 23-25 uwanja wa Chamanzi Complex na Azam ina kazi ya kupindua meza kibabe ili kusonga mbele, kuanzia goli 2 au zaidi zitaipa tiketi timu hiyo kusonga mbele.

Kwenye michuano ya Caf, Azam ndio timu pekee kupoteza mchezo wa awali kutoka Tanzania baada ya klabu ya Yanga kutoa sare ya 1-1 na Township Rollers, Simba 0-0 US de Dongo na Kmc 0-0 AS Kigali.

Author: Bruce Amani