Bayern yaweka pengo la pointi nne kileleni

126

Bayern Munich wamejiweka sawa kileleni mwa Bundesliga baada ya bao la Niklas Süle katika dakika ya 75 kuwapa ushindi wa 1 – 0 dhidi ya wasumbufu Werder Bremen waliomaliza mechi na wachezaji kumi uwanjani.

Kipa wa Bremen Jiri Pavlenka alizuia kombora la Serge Gnabry na Robert Lewandoswki akapiga shute nje ya lango kabla ya shuti la Niklas Süle kuingia wavuni kwa kumgonga Davy Klaassen.

Beki wa Bremen Milos Veljkovic alipewa alitimuliwa uwanjani katika dakika ya 58 kwa kupewa kadi ya pili ya njano.

Nambari mbili Borussia Dortmund watacheza Jumapili dhidi ya Freiburg.

Bayern wamesalia na mechi nne msimu huu wakati wakilenga kupata taji la saba mfululizo la Bundesliga.

Stuttgart yamtimua Weinzierl

Kwingineko Jumamosi, Eintracht Frankfurt walikwamilia nafasi ya nne bila hata kucheza baada ya nambari tano Borussia Monchengladbach kuzabwa 2-1 nyumbani dhidi ya nambari tatu RB Leipzig. Monchengladbach wanabaki na pointi 51 moja nyuma ya Frankfurt ambao watacheza ugenini Jumatatu dhidi ya Wolfsburg

Wakati huo huo, Stuttgart wamempiga kalamu kocha wao Markus Weinzierl baada ya kichapo cha 6-0 dhidi ya Augsburg. Mjerumani huyo alpoteza mechi 15 kati ya 23 tangu alipochukua usukani Oktoba.

Author: Bruce Amani