Dortmund yaweka hai matumaini ya kubeba ubingwa

101

Borussia Dortmund wameendeleza vita vya ubingwa wa ligi kwa kupata ushindi wa 4 – 0 dhidi ya Freiburg na kuwakaribia vinara Bayern Munich na pengo la pointi moja.

Nahodha Marco Reus alilazimika kucheza na maumivu ili kuipa motisha timu yake na kuisaidia kwa kufunga bao moja na kutoa assist mbili.

Aliogongwa goti baada ya kukabiliana na Janik Haberer baada ya kuifungia Dortmund bao la pili.

Jadon Sancho alifungua ukurasa wa mabao kabla ya mkwaju wa Mario Goetze na penalty ya Paco Alcacer kukamilisha kichapo hicho.

Reus anasema bado wanaamini kuwa wanaweza kuwa mabingwa na wanataka kuwawekea Bayern mbinyo hadi siku ya mwisho ya msimu.

Author: Bruce Amani