Ivory Coast hoi mikononi mwa Algeria

146
Ivory Coast imeondoshwa rasmi kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika Afcon 2019 baada ya kufungwa 4 – 3 na Algeria. Ni baada ya mchezo wao wa robo fainali uliofanyika leo Alhamis Julai 11 na kushuhudia dakika 120 zikimalizika kwa sare ya goli 1-1.
Matokeo hayo yanaifanya Ivory Coast kupoteza kuishia robo fainali huku ikipoteza rekodi nzuri dhidi ya Algeria kwani kabla ya mtanange wa leo, Tembo hao walikuwa wakiongoza kwa michezo mitatu.
Katika hatua ya matuta ilishuhudiwa penati ya Wilfred Bonny na Serey wote wa Ivory Coast wakikosa penati na kiungo mshambuliaji wa  Algeria Bounedjah nae alikosa mkwaju wa penati.
Mbali na kuondoshwa  kwa Ivory Coast watajilaumu wenyewe kwa kupoteza nafasi nyingi za wazi katika kipindi cha kwanza kabla ya Algeria kuongoza goli kunako kipindo cha kwanza dakika ya 26 na Coast kusawazisha dakika ya 62.
Algeria inasonga mbele kufika nusu fainali ambapo atakutana na Senegal.

Author: Bruce Amani