Kocha Tuchel aongezwa mkataba wake PSG hadi 2021

113

Kocha wa mabingwa wa Ufaransa Paris Saint Germain Thomas Tuchel amerefusha mkataba wake na klabu hiyo hadi Juni 30 2021.
Mjerumani huyo alichukua usukani wa klabu hiyo ya Ligue 1 Juni 2018 na kuiongoza kutwaa taji la Ufaransa msimu huu.
Hata hivyo, PSG kwa mara nyinginge ilishindwa kupata mafanikio waliyotaka katika Champions League baada ya kuondolewa na Manchester United katika hatua ya 16 za mwisho.
PSG pia walizabwa katika fainali ya Kombe la Ufaransa walipopoteza dhidi ya Rennes kupitia mikwaju ya penalti.
“Ningependa kumshukuru mwenyekiti na klabu nzima kwa imani yao kwangu na makocha wenzangu.” Alisema Tuchel, 45.
“Hili linaongeza nguvu lengo langu la kuiweka klabu hii katika kiwango cha juu kabisa kupitia kazi ngumu.”

Author: Bruce Amani