Mahrez aiadhibu Nigeria na kuipeleka Algeria fainali

232
Shuti la mpira freekick la dakika za nyongeza lilopigwa na Winga wa Manchester City Riyad Mahrez limeipeleka Algeria fainali ya Afcon 2019 nchini Misri katika mchezo uliochezwa dimba la Kimataifa Cairo.
Mchezo ukiwa unaelekea kwenye dakika za nyongeza Mahrez amekatisha ndoto za Nigeria kunyakua kombe la Afcon kwa mara ya 5 sasa.
Sura ya mtanange huo ilibadilika baada ya William Troost-Ekong kujifunga upande wa Algeria kabla ya Odion Ighalo kusawazisha kwa penati baada ya matumizi ya VAR. Goli la Ighalo kwa Algeria linakuwa goli la pili Algeria kufungwa tangu kuanza kwa michuano hiyo, inaonyesha namna safu nzuri ya ulinzi ilivyo.
Algeria itakutana na Senegal kwenye kilele cha mashindano hayo siku ya Ijumaa Julai 19.
Algeria imechukua taji la Afcon mara moja mwaka 1990 na kama wataweza sasa litakuwa taji lao la pili wakati Senegal hawana kitu.
Senegal licha ya kupita vizazi vya dhahabu bado Kombe la Afcon halipo kabatini, inawezekana kizazi hiki cha akina Sadio Mane, Idrissa Gana Gueye, Kalidou Koulibaly, Kouyate vikaweza.

Author: Bruce Amani