Makocha waendelea kuathiriwa na matokeo ya Afcon
Makocha wawili zaidi wamepoteza kazi zao na mwingine anatarajiwa kibarua kuota nyasi katika siku za hivi karibuni wakati hali hiyo ikijitokeza katika mashindano ya fainali za mataifa ya Afrika, AFCON, nchini Misri kwa timu ambazo hazikutimiza matarajio ya mashabiki wake.
Paul Put aliondolewa na Guinea jana Jumatatu licha ya kukifikisha kikosi hicho katika awamu ya timu 16 bora wakati Richardo Mannetti mkataba wake haukurefushwa baada ya Namibia kupoteza michezo yake yote mitatu ya makundi.
Majaaliwa ya bingwa mara mbili wa taji hilo la Afrika Herve Renard akiwa na kikosi cha Morocco pia inaonekana kuelekea mwisho ambapo vyombo vya habari nchini humo jana vilipigia upatu kuondoka kwake na kocha huyo kuweka hali yake ya baadaye katika hali ya kutojulikana kwa kutoa taarifa tata.
Kwa ombi langu, nimekutana na Fouzi Lekjaa, rais wa shirikisho la kandanda la Morocco, amesema Renard.