Morocco yapata ushindi wa jioni dhidi ya Afrika Kusini

170

Morocco ilihitaji ushindi wa jioni tena mwembamba wa goli 1- 0 dhidi ya Afrika ya Kusini katika mchezo wa kundi D wa mashindano ya Kimataifa Afrika Afcon na kutinga hatua ya mtoano kama kinara wa kundi hilo.

Ukiwa mchezo wa tatu wa michuano ya Kimataifa Afrika Afcon Morocco goli lao limefungwa na nahodha wa kikosi hicho M’bark Boussoufa kunako dakika ya 89 ya mchezo, ambapo mpaka dakika 90 zinakamilika Morocco 1-0 A.Kusini

Ushindi huo unaifanya Simba wa Milima ya Atlas kumaliza na alama 9 wakati Ivory Coast ikimaliza na alama sita baada ya kuibuka na ushindi mechi mbili, Afrika Kusini alama tatu na Namibia alama 1.

Morocco na Ivory Coast tayari zimekata tiketi ya raundi ya 16 bora wakati Afrika Kusini wakisubiri matokeo ya mchezo wa Kenya, Guinea pia.

Author: Bruce Amani