Napoli yachelewesha karamu ya Juventus ya ubingwa wa ligi

148

Napoli ilitoka sare ya 1 – 1 na Genoa jana Jumapili na kuhakikisha kuwa Juventus itasubiri kwa wiki moja nyingine kubeba ubingwa wa nane mfululizo wa ligi ya Italia. Mabingwa hao wana faida ya mwanya wa pointi 20 dhidi ya nambari mbili Napoli huku ikiwa imesalia michuano saba msimu kukamilika. Juventus ambao waliwabwaga AC Milan 2 – 1 Jumamosi, walihitaji Napoli kushinda ili kunyakua taji la Serie A kwa mara ya 35, kabla ya mchuano wao wa mkondo wa kwanza war obo fainali ya Champions League dhidi ya Ajax wiki hii.

Matokeo ya sare katika mchuano wa wikiendi ijayo dhidi ya SPAL yatatosha kuwahakikishia vijana hao wa Massimiliano Allegri taji ambalo litakuwa la kwanza nchini Italia kwa mchezaji nyota Cristiano Ronaldo.

Awali, Atalanta ilipoteza nafasi ya kusonga hadi nafasi ya nne ambayo ni tiketi ya Champions League, baada ya AC Milan kutoka sare ya 0 – 0 katika uwanja wa San Siro. Inter wako katika nafasi ya tatu na pointi 57 – ikiwa ni pengo kubwa sana la pointi 27 nyuma ya Juventus – huku Milan wakiwa nyuma ya mahasimu wao hao wa jiji na mwanya wa pointi tano.

Author: Bruce Amani