Newcastle yavuruga mipango ya Man City kubeba ubingwa

159

Rafa Benitez hajawahi kushinda ubingwa wa Ligi ya Premier katika miaka yake sita akiwa na Liverpool lakini ameipa timu yake hiyoy a zamani msaada mkubwa sana katika jitihada yake ya kumaliza ukame wa miaka 29 bila kuweka mikono yake kwenye tuzo hiyo kubwa ya kandanda la England.

Newcastle, inayokabiliwa na matatizo ya majeruhi kikosini na inayotishiwa kushuka daraja, na ambayo sasa inaongozwa na Benitez, ilisababisha mojawapo ya matokeo ya kushangaza sana msimu huu kwa kutoka nyuma na kuinyamazisha Manchester City 2 -1 Jumanne usiku. City sasa wako nyuma ya vinara Liverpool na pengo la pointi nne ambao wana fursa ya kurefusha uongozi wao hadi pointi saba kwa kuwazaba Leicester Cict uwanjani Anfield Jumatano. Kutakuwa na mecjhi 14 kwa timu zote mbili baada ya hapo.

Ulikuwa usiku mbaya kwa timu za Manchester. Kocha wa muda wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer alikuwa akilenga kuwa kocha wa kwanza katika Premier League kushinda mechi saba mfululizo lakini Burnley wakavuruga mpango huo. Timu yake ilipambana kutoka nyuma 2 -0 na kulazimisha sare ya 2 – 2. United wako nyuma ya nambari tano Arsenal na mwanya wa pointi mbili. Arsenal waliwashinda Cardiff 2 – 1. Nambari nne Chelsea itacheza Jumatano ugenini dhidi ya Bournemouth, katika kinyang’anyiro kikao cha kuwania nafasi nne bora.

Author: Bruce Amani