Özil na Kolasinac warejea kuivaa Burnely

103

Kocha wa Arsenal Unai Emery amesema wachezaji wake wawili Mesut Ozil na Sead Kolasinac wapo sawa kiakili kucheza mechi ya Jumamosi dhidi ya Burnley. Wawili hao waliachwa kwenye ushindi wa mchezo wa ufunguzi dhidi ya Newcastle United baada ya kukumbwa na tukio la kuvamiwa na vibaka mwezi Julai.

Tangu muda huo kiungo mshambuliaji Ozil na beki wa kulia Kolasinac hawajawai kufanya mazoezi na wenzao mpaka katikati ya wiki hili. “Ni habari njema kwetu kwa kuwa watatusaidia kwenye michezo mbalimbali,” Alisema Emery kocha wa Arsenal.

“Lengo langu lilikuwa kuwafanya wako vizuri kiakili kwa asilimia 100 ili wawekeze nguvu zao kwenye mpira kuliko kuwalazimisha kucheza kabla ya akili yao kutengemaa.” Aliongeza

Msimu huu Arsenal imefanya usajili mkubwa huenda kurejea kwa Mesult Ozil na Kolasinac kusilete mabadiliko makubwa ndani ya kikosi hicho, Ceballos, Luiz, Pepe ni miongoni mwa majina yanayotegemewa kufanya vyema msimu huu.

Author: Bruce Amani