Penalti ya Messi yaipa Barcelona ushindi dhidi ya Valladolid

128

Lionel Messi alifunga penalty moja na akapoteza nyingine wakati Barcelona ikipata ushindi wa 1 – 0 dhidi ya Real Valladolid na kujiimarisha kileleni mwa La Liga na pengo la pointi saba.

Messi alifunga bao lake la 30 katika msimu wa 2018-19 wakati alisukuma kambani mkwaju wa penalty baada ya Michel kumuangusha Gerard Pique kwenye eneo hatari.

Barcelona walipewa penalty ya pili wakati nguvu mpya Philippe Coutinho aliangushwa na Kiko Olivas, lakini mara hii kipa Jordi Masip aliokoa shuti la Messi.

Masip pia aliokoa mipira kadhaa na kuwanyima Luis Suarez na Messi nafasi ya kufunga bao.

Matokeo hayo yanaiwacha Barcelona kileleni na mwanya wa pointi sana mbele ya nambari mbili Atletico Madrid, waliopata ushindi wa 1- 0 dhidi ya Rayo Vallecano mapema Jumamosi. Bao la Atleti lilitiwa kimiani na mshambuliaji Antoine Griezmann

Real Madrid wako katika nafasi ya ttau, pointi mbili nyuma ya Atletico, na watacheza mechi yao ya ziada Jumapili dhidi ya Girona

Author: Bruce Amani