Senegal yatinga fainali kwa kuifunga Tunisia

160
Senegal imefuzu kuingia fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa Afrika – Afcon 2019 baada ya kupata ushindi (1-0) dhidi ya Tunisia katika muda wa nyongeza baada ya suhulu kwenye dakika 90.
Tmu zote zilipata penati kwenye dakika za kawaida na kushindwa kuzitumia vyema kabla ya mlinzi wa klabu ya Gent ya Ubeligiji Dylan Bronn, 24, kujifunga kwa kichwa kunako dakika ya 101 baada ya mpira kumgonga kichwani baada ya makosa ya Mlinda mlango wake
Matokeo hayo yanaifanya Senegal kukutana kati ya Algeria ama Nigeria katika fainali ya mashindano hayo.
Matumizi ya VAR yametumika kutoa utata kwenye dakika za lala salama baada ya Mwamuzi kudai Gana Gueye aliugusa mpira kwa mkono akiwa katika hatua ya kuokoa.
Hii ni mara ya kwanza kwa Senegal kufika hatua ya fainali tangu mwaka 2002 licha ya kwamba haijawai kutwaa taji jili tangu kuanzishwa kwake.

Author: Bruce Amani